Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao. Geita. Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM). Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao. Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa. Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa. Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kiten...
Matukio, Habari za Uhakika